BARAZA LA MADIWANI WILAYANI TANGANYIKA LAIOMBA SERIKALI KUKAMILISHA MIRADI VIPORO YA MAENDELEO ILI WANANCHI KUENDELEA KUWA NA IMANI NA SERIKALI.



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Tanganyika Katavi
BARAZA la madiwani Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,limeiomba serikali kuhakikisha inakamilisha miradi ya maendeleo katika kata mbalimbali ili kuwanufaisha wananchi kiuchumi na kimaendeleo.
Madiwani wa Baraza la madiwani wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda wakiwa katika kikao(PICHA NA.Issack Gerald)
Aliyesimama ni Mwenyekiti wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw.Hamad Hassan Mapengo(PICHA NA.Issack Gerald)
                                                          

Baraza limetoa ombi hilo katika kikao chake ambacho kimefanyika leo katika ukumbi wa Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda uliopo Mpanda Mjini.
Wamesema kuwa kukamilika kwa miradi kutapelekea wananchi kuwa na imani kwa serikali yao katika kuwaletea maendeleo huku madiwani wa baraza hilo wakitaka kutoibuliwa miradi mipya kabla ya kukamilisha miradi viporo.
Katika kujibu hoja za madiwani wa Baraza hilo,Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Bw. Ngalinda Hawamu Ahmada amesema,serikali itaendelea kukamilisha miradi viporo iliyokwishaibuliwa ikiwa ni sambamba na kuanzisha miradi mipya ya maendeleo.
Katika hatua nyingine Bw. Ahmada amesema asilimia 5 ya mapato kwa ajili ya kuwawezesha vijana inaandaliwa ni kuwa kichocheo cha maendeleo.
Wilaya ya Tanganyika bado ina matatizo ya uhaba wa maji,waganga,wakunga na wauguzi,walimu katika shule za msingi na sekondari huku miundombinu ya barabara nayo ikitakiwa kukarabatiwa.
Wilaya ya Tanganyika ina jumla ya kata 16 ambapo miongoni mwa kata hizo ni pamoja na kata za Mishamo,Karema,Ipwaga,Ilangu,Bulamata,Mpanda ndogo na makao makuu ya Wilaya ya Tanganyika kata ya Majalila.
Endelea kuhabarika P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA