SHIRIKA LA UNHCR LAKABIDHI GARI LA SHILINGI MILIONI 150 KWA JESHI LA POLISI WILAYANI TANGANYIKA,WAAHIDI KUTOA MAFUTA NA KULIKARABATI LINAPOHARIBIKA,JESHI LA POLISI KATAVI LAAGIZWA KUIMARISHA USALAMA.



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama- Katavi
SHIRIKA la Wakimbizi duniani UNHCR limekabidhi gari mpya kwa jeshi la Polisi Wilayani Tanganyika Mkoani Katavi,ili kurahisisha na kuongeza utendaji kazi wa jeshi hilo katika kuimarisha usalama wa raia na mali zao.
Picha ya Pamoja ya Jeshi la Polisi Baada ya UNHCR kukabidhi gari kwa Jeshi La Polisi Wilayani Tanganyika(PICHNA NA.Issack Gerald),wa Kwanza kutoka kulia ni kamanda wa Jeshi Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda
                               

Akikabidhi gari hilo aina ya Toyota Land Cruiser lenye thamani ya Shilingi Milioni 150,Mkuu wa Ofisi za Shirika la UNHCR Wilayani Mpanda Bw.Deo  Rwasamanzi,amesema kuwa UNHCR wametoa gari hilo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kurahisha usafiri kwa jeshi la Polisi ili kufanya kazi kwa ufanisi katika kuimarisha usalama.
Aidha Bw. Rwasamanzi amesema shirika la UNHCR litaendelea kutoa mafuta na ukarabati wa gari hilo na huduma nyingine zinazohitajika ambapo hata hivyo ametoa wito kwa jeshi la polisi kulitumia vizuri gari hilo ili lidumu kwa muda mrefu.
Kwa upande wake Dkt Yahaya Hussein Mganga Mkuu wa Mkoa wa Katavi kwa niaba ya Katibu tawala mkoa wa Katavi Kamishna Paul Chagonja ambaye alikuwa Mgeni rasmi katika hafla hiyo ya makabidhiano ya gari hilo ambayo yamefanyika  katika Ofisi za UNHCR  zilizopo katika kata ya Mishamo ,ameliagiza Jeshi la polisi kuhakikisha usalama unaimarishwa ikiwa ni sambamba na matumizi sahihi ya gari hilo.
Aidha Dk Hussein mbali na kulipongeza Shirika la UNHCR kwa msaada huo pia ametoa wito kwa mashirika mengine kujitokeza kuunga mkono juhudi za serikali kuleta maendeleo na kuimarisha usalama.
Mkuu wa kituo cha Polisi Wilayani Tanganyika Amon Charles Mimanta baada ya kukabidhiwa gari hilo amesema,gari hilo litasadia jeshi la polisi kufika mahali ambapo walikuwa hawafiki kutokana na upungufu wa magari.
Wilaya ya Tanganyika Mkoani Katavi Agosti mwaka huu pia walikabidhiwa gari la wagonjwa ambapo takribani Magari 5 yamekwishakabidhiwa kwa serikali ya Mkoa wa Katavi kutoka kwa Shirika la UNHCR.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na viongozi na watumishi mbalimbali wakiwemo  Mkuu wa Makazi Mishamo Bw.Joseph Hossea,Kamati za ulinzi na usalama Wilaya ya Tanganyika  na Mkoa ,baadhi ya watumishi wa UNHCR na uongozi wa kata ya Mishamo.
Miongoni mwa uharifu ambao umekuwa ukitajwa kutokea mara kwa mara katika Wilaya ya Tanganyika ni pamoja na wizi mdogomdogo wa mali za raia.
Endelea kuhabrika zaidi kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA