MKUU WA MKOA WA KATAVI APOKEA SHILINGI 500,000/= KUTOKA MUKABUBINGA KWA AJILI WAATHIRIKA TETEMEKO LA ARDHI KAGERA,FEDHA ILIYOCHANGWA YAFIKIA MIL. 13,344,600 KUWASILISHWA KAGERA JUMATATU.

Na.Issack Gerald Bathromeo - Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral mstaafu Raphael Muhuga amepokea Shilingi laki tano kutoka kwa MUKABUBINGA ambao ni Umoja wa wanakagera waishio Wilayani Mpanda ambapo fedha hiyo ni kwa ajili ya kuwachangia waathirika wa tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera.
Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Katavi na Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda(PICHA NA.Issack Gerald)
Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Mugoya Muhuga(PICHA NA.Issack Gerald)                   

Mmoja wa viongozi wa umoja huo Bw.Rugalema Gelasius akiwasilisha taarifa kwa niaba ya umoja huo,amesema walipokea kwa masikitiko makubwa ya tukio la tetemeko la ardhi lililosababisha vifo vya watu 17,majeruhi na kusababisha uharibifu wa mali,makazi ya watu,shule na vituo vya huduma za afya. 
MUKABUBINGA ni neno ambalo limeundwa na Wilaya za Muleba,Karagwe,Bukoba,Biharamulo na Ngara zote za Mkoa wa Kagera.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Mstaafu Raphael Muhuga mbali na kuupongeza umoja wa wanakagera hao,amesema mpaka sasa zaidi ya shilingi milioni 13,344,600 zimekwishapatikana ili kuwasaidia waathiriwa ambapo fedha hiyo inatarajiwa kuwasilishwa Mkoani Kagera Jumatatu Ijayo ya Oktoba 10,2016.
Wakati huo huo wana umoja wengine wa MUKABUBINGA wanaotoka wilaya mbalimbali za Mkoa wa Kagera mbali na kueleza na tetemeko hilo,wameziomba taasisi nyingine na mtu mmoja mmoja kujitokeza kuwachangia walioathirika.
Umoja wa wanakagera waishio Mpanda MUKABUBINGA wapatao 29 walioanzisha umoja huo mwaka 2002,wamekabidhi fedha hiyo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa na kuhudhuriwa Katibu tawala wa Mkoa wa Katavi sambamba na waandishi wa habari Mkoani Katavi.
Tukio la tetemeko la ardhi lilitokea Septemba 10 mwaka huu ambapo pia mbali na kuathiri upande wa Tanzania,pia nchi zikiwemo Uganda na Kenya ziliguswa na tukio hilo.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA