TRA RUKWA NA KATAVI YAENDESHA SEMINA KUHUSU MFUMO MPYA ULIPAJI KODI


Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
WAFANYABIASAHARA mikoa ya Rukwa na Katavi wametakiwa kutofumbia macho vikwazo vinavyotokana na mfumo mpya wa ulipaji kodi na badala yake watoe taarifa na maoni ili kuangalia kama kuna uwezekano wa kuondoa vikwazo hivyo ili wafanye biashara zao kwa uhuru.
                              

Wito huo umetolewa jana na  Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Mpato Tanzania (TRA) Bw.Enosi Mjimba wakati wa Semina ya mafunzo ya elimu ya mlipa kodi kwa mfanyabiashara semina ambayo ilifanyika Mpanda Mjini.
Alisema kuwa mfumo wa ulipaji kodi ulioanzia Julai mosi mwak huu kwa mwaka wa fedha2016/2017 umeleta mabadiliko katika sheria ya Kodi ya Mapato,Kodi ya ongezeko la thamani,Sheria ya mamalaka ya Mapato Tanzania,Sheria ya usimamizi wa kodi,Sheria ya usimamizi wa Vyombo vya moto na Sheria ya VETA.
Kwa upande wake Afisa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi mkoa wa Rukwa na Katavi Bw.Philipo Eliaminy amewataka wenye tabia ya kuuziana vyombo vya usafiri kama pikipiki mitaani wafike katika Ofisi za Mamlaka ya Mapato Tanzania na kubadili majina ya usajili ili kuepuka gharama zinazotokana na kulipa madeni aliyokuwa akidaiwa aliyemuuzia kwa kuwa jina la mdaiwa litaonekana la mmiliki wa awali.
Nao baadhi ya wafanyabiashara wakiwemo Mwenyekiti wa Jumuiya ya wafanyabiasahara Tanzania Tawi la Katavi Bw.Aman Mahellah na Mwenyekiti wa Wenye viwanda,kilimo na Biasahara Wilayani Mpanda Bw.Shabir Dalla mawesema kuwa miongoni mwa changamoto zinazotakiwa kufanyiwa kazi haraka na TRA ni pamoja na kuimarisha mitandao ya Mashine za EFDs,kutoa elimu mara kwa mara ya mlipa kodi kwa mfanyabiashara na kuwakilisha matatizo ya wafanyabiasahara ngazi za juu ili yafanyiwe kazi haraka.
Katika Shilingi Trilioni 29.5 za makadirio ya serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 zinazotarajiwa kutumiwa na serikali katika uendelezaji wa shghuli mbalimbali,Mamalaka ya Mapato Tanzania TRA imepangiwa kukusanyanya Shilingi Trilioni 15.1.
Wafanyabiasahara wapatao 100 walishiriki katika semina ya mafunzo ya elimu ya mlipa kodi ambapo hii ni semina ya kwanza kufanyika Mkoani Katavi Tangu Mwaka wa fedha 2016/2017 uanze mwezi Julai mwaka huu kuhusu mfumo mpya wa elimu kwa mlipa kodi unaowahusisha wafanyabiasahara.
Mhariri:Issack Gerald Bathromeo
Habarika Zaidi  na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM                

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA