KAMATI TENDAJI MRADI ELIMU JUMUISHI MKOANI KATAVI NA UJUMBE WA UGENI KUTOKA MIKOANI WAFANYA KIKAO KUJADILI MAHITAJI YA WATOTO WENYE ULEMAVU


Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Katavi

JAMII Mkoani Katavi imetakiwa kushiriki ipasavyo kuwafichua watoto wenye Ulemavu ili wapatiwe elimu kama watoto wengine wasio na ulemavu.


Wito huo umetolewa leo na Verhan Bakari ambaye ni mwezeshaji utathmini na utafiti wa mradi wa elimu Jumuishi  kutoka chuo cha Maendeleo ya Jamii Tengeru Arusha ambaye amekuja  Mkoani Katavi kutathmini mafanikio na changamoto pia mikakati inayotakiwa kuchukuliwa ili kuendeleza mradi wa elimu Jumuishi katika Mikoa ya Rukwa na Katavi.

Akizungumza na Kamati tendaji ya kulea baraza la watoto wenye mahitaji maalumu Wilayani Mpanda katika Ofisi za Kamati hiyo zilizopo Mpanda Mjini,Bw.Bakari amesema kila mtu kwa nafasi yake ni wajibu wake kuhakikisha watoto wenye ulemavu hawanyanyapaliwi kwa namna yoyote hususani katika sekta ya elimu au mahitaji ya msingi anayotakiwa kupatiwa.

Kwa upande wake Mratibu wa mradi wa elimu Jumuishi Mkoani Katavi Bw.Raphael Fortunatus,mbali na kutoa wito kwa wazazi na walezi kuwapeleka shule watoto wenye uleamvu,amesema mafanikio ya mradi huo ambayo yamepatikana kwa kipindi cha mwaka 2015/2016 ni kuongezeka wanafunzi walioandikishwa shuleni,ambapo kuanzia mwezi Januari 2016 mpaka mwezi huu,zaidi ya watoto wenye ulemavu 90 wameandikishwa ikilinganishwa na watoto wapatao 50 waliokuwa wakiandikishwa kwa kipindi cha nyuma kabla ya mradi kuanza 2012.

Bw.Fortunatus ambaye pia ni Mwalimu wa Shule ya Msingi Azimio anayefundisha wanafunzi wenye ulemavu,ametaja baadhi ya maeneo ambayo wanafunzi wenye ulemavu wameongezeka kuandikishwa shuleni kuwa ni pamoja na Kata ya Mwamkulu,Kakese na Manispaa ya Mpanda ambapo pia amesema kwa sasa maeneo mengi yana majengo rafiki kwa mtoto mlemavu ikiwemo vyoo na madarasa.

Naye Serapioni Rwegasila ambaye ni mzazi katika kamati ya kulea baraza la watoto Wilayani Mpanda,amesema bado kuna wazazi na walezi hawatambui umuhimu wa mtoto mlemavu kupatiwa elimu na ameomba elimu zaidi itolewe kwa wazazi hao wasiotambua umuhimu huo.

Mradi wa elimu Jumuishi ulioanza mkoani Katavi mwaka 2012 unawezeshwa na Shirika la IFI lenye muunganiko wa washirika watatu ambao ni Internation Aid Services(IAS),Free Pentecoastal Church of Tanzania(FPCT) na International Centre Of Disability(CID).

Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Kwa maoni au Ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Mwandishi na Mhariri: Issack Gerald Bathromeo Mashama

 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA