MKUU WA WILAYA YA MPANDA AHAMASISHA HARAMBEE KUWACHANGIA WAATHIRIKA WA TETEMEKO LA ARDHI MKOANI KAGERA


Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama- Mpanda Katavi

MKUU wa Wilaya ya Mpanda Bi.Lilian Charles Matinga,ametoa wito kwa wakazi wa Wilaya ya Mpanda kujitokeza kwa hiari katika harambee ya kuwachangia wakazi wa Mkoa wa Kagera walioathiriwa wa tetemeko la ardhi Septyemba 10 mwaka huu.

Mkuu wa Wilaya Bi.Lilian ambaye pia ndiye mwenyekiti wa kamati ya maafa Wilayani Mpanda,ametoa rai hiyo, wakati akizungumza na Mpanda Radio asubuhi ya leo ambap[o amesema kuwa michango hiyo si lazima iwe fedha bali pia hata vitu kama mabati,saruji na vifaa vingine vya ujenzi vinapokelewa.

Amesema Mpaka sasa barua za harambee zimesambazwa kwa taasisi mbalimbali wilayani Mpanda zaidi ya 68 ambapo pia wengine wenye moyo wa kuchangi wanaweza kuwasilisha michango yao kupitia viongozi wa mitaa na vijiji pia kupitia kwa makatibu wa kamati za maafa Wilaya ambao ni Wakurugenzi wa Halmshauri ya Wilaya yaManispaa ya Mpanda na Nsimbo.

Wakati huo huo amesema kwa wakazi walio Nje ya Mpanda wanaruhusiwa kuchangia kupitia namba za mitandao ya mawasiliano ambazo zimeambatanishwa katika barua za maombi ya michango hiyo.

Katika hatua nyingine amesema michango itakayokuwa imepatikana inatarajiwa kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Katavi Meja Jeneral Raphael Mugoya Muhuga na hatimaye kusalishwa kwa Waziri Mkuu wa Tanzania Mh.Kassim majaliwa ili michango hiyo iwasilishwe Mkoani Kagera kwa wathirika.

Makumi ya watu walipoteza maisha katika teemeko hilo huku mamia wakijeruhiwa na idadi ya maelfu ya nyumba zikiharibiwa vibaya wakati huo huo shule na vituo vya huduma za afya vikiharibiwa vibaya.

Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Kwa maoni au Ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Mwandishi na Mhariri: Issack Gerald Bathromeo Mashama

 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA