UKOSEFU WA FEDHA,WAZEE KATAVI WASHINDWA KUHUDHURIA MAADHIMISHO YA KESHO SIKU YA WAZEE DUNIANI YATAKAYOFANYIKA MKOANI MBEYA



Na.Issack Gerald Bathromeo mashama-Katavi
UMOJA wa wazee Mkoani Katavi umeshindwa kupeleka wawakilishi katika maadhimisho ya Siku ya wazee Duniani yanayotarajiwa kufanyika kitaifa kesho Mkoani Mbeya.
Moja ya mikitano iliyokuwa ikijadili maslahi ya wazee(PICHA NA Issack Gerald )Septemba 2014
                                           

Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Umoja huo Mkoa Bw.Benard Sangija na katibu wa Umoja huo Bw.Marius Bagaya, wakati wakizungumza na Mpanda Radio katika Ofisi ya umoja huo ziliyopo Mpanda Mjini.
Kwa mjibu wa Umoja huo,Halmshauri tano za Mkoa wa Katavi zimetoa taarifa katika umoja huo kuwa,mwaka huu Halmashauri hazina fedha kuwawezesha wazee kwenda kushiriki maadhimisho ambapo pia mwaka 2015 Halmshauri zilishindwa kufanya hivyo.
Wakati kesho ikiwa ni siku ya wazee Duniani,Katika Mkoa wa Katavi baadhi ya wazee Manispaa ya Mpanda akiwemo Bi.Fatma Saleh Mkazi wa Kata ya Majengo(64) wamesema, matatizo makubwa yanayowakabili na kuwa tishio kwa wazee ni pamoja na suala la ukosefu wa maji hali inayowapa shida kubwa sana ikiwa hawana nguvu ya kugombania maji na vijana wenye nguvu.
Mbali na suala la maji, wamesishauri Halmshauri ya Maniaspaa ya Mpanda kuongeza juhudi za kuzoa taka ambazo kwa sasa wamesema zimelundikana katika makazi yao na kuhofia kukumbwa na magonjwa ya mlipuko ikiwemo Kipindupindu wakiongeza kuwa kutozolewa taka,Halmashauri inakuwa haijaunga mkoano ipasavyo juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli anayetaka Tanzania iondokane na kuzagaa ovyo kwa uchafu.
Katika hatua nyingine,baadhi ya wazee Mkoani Katavi wameonekana kusikitishwa na hatua ya kustaafu kwa Daktari Patrick Mwita kwa mjibu wa sheria na kanuni za utumishi wa umma,wakisema kuwa hawana matumaini ya kupata daktari mwenye upendo kwa wazee kama daktari Patrick ambaye alikuwa akiwahudumia wazee ipasavyo katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda katika huduma zinazowalenga wazee.
Wakati huo huo wazee wamesema baadhi ya ahadi zilizokuwa zimeahidiwa katika maadhimisho ya mwaka 2014 yaliyofanyika kitaifa mkoani Katavi ilikuwa ni pamoja na wazee kupewa eneo la ujenzi wa Ofisi za wazee Mkoani Katavi,kupewa pensheni ili kujikimu na maisha ambapo mpaka sasa ahadi hizo wamesema hazijatekelezwa na kutokana na hali hiyo,wameiomba serikali kuwaangalia namna ya kuwasaidia wazee hao.
Hata hivyo miongoni mwa mafanikio makuu baada ya maadhimisho ya mwaka 2014 Mkoania Katavi ni pamoja na wazee kupewa kipaumbele katika suala la matibabu,kuboreshwa kwa wizara ya afya kutoka Wizara ya afya na ustawi wa jamii miaka ya zamani na kuwa Wizara ya afya,maendeleo ya Jamii,Jinsia wazee na watoto.
Katika sensa ya mwaka 2012 ya watu na makazi,Mkoa wa Katavi ulibainika kuwa na jumla ya wazee wapatao 5000 ambapo mpaka sasa jumla ya mabaraza 20 ya wazee katika maeneo mbalimbali ya Mkoani Katavi yameundwa.
Mkoa wa Katavi ni miongoni mwa mikoa ya Tanzania bara ambayo kitaifa iliwahi kuandaa maadhimisho ya siku ya wazee duniani yaliyoadhimishwa Oktoba mosi mwaka 2014 Wilayani Mpanda.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni,ushauri au ukiwa n ahabari yoyote,tutumie kupitia email ya Ofisi p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA