WAFANYABIASAHARA MANISPAA YA MPANDA WAPEWA SIKU 6 KUONDOKA MASOKO YASIYO RASMI KABLA YA NGUVU KUTUMIKA.




Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
WANANCHI wanaofanya biashara katika masoko yasiyo rasmi Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,wametakiwa kuondoka na bidhaa zao wenyewe kwa hiari kabla ya Septemba 5 mwaka huu kuondolewa kwa nguvu.
Katika Picha Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Nzyungu(PICHA NA.Issack Gerald)
Miongoni mwa wafanyabishara wanaopigwa marufuku soko lisilo rasmi lililopo Ujenzi Machinjioni Mpanda hotel.
                                                   

Kauli hiyo imetolewa leo kwa vyombo vya habari na Mkurugenzi Mtendaji Manispaa ya Mpanda Bw.Michael Fransis Nzungu,kupitia kwa Afisa habari wa Manispaa hiyo Bw.Donald Pius.
Aidha Nzungu amesema kuwa wananchi wanatakiwa kuzingatia na kuheshimu sheria za mipango miji,kwa kufanya shughuli zao za kila siku katika maeneo yaliyo sahihi ili kuepuka usumbufu unaoweza kujitokeza.
Mkurugenzi katika taarifa yake amesema wananchi waliopo katika kata ya Mpanda Hotel,Kawajense na Nsemulwa wamekuwa wakivunja sheria za mipango miji kwa kuanzisha masoko katika maeneo yasiyo rasmi na hivyo kuharibu mpango mzima wa Mji wa Mpanda.
Aidha amesema kuanzia Septemba 5 mwaka huu,hataruhusiwa mtu yeyote kufanya biashara katika maeneo yasiyo rasmi.
Masoko yasiyo rasmi ambayo wafanyabiashara wametakiwa kuondoka na kwenda katika masoko rasmi ni wanaofanya biashara maeneo ya Ujenzi Machinjioni na Kawajense Uenyejini.
Kwa upande wa wafanyabiashara wanaofanya biashara zao eneo la Nsemulwa Migazini,wametakiwa kuhamia kwa muda kwenye soko lililopo jirani na Tanki la maji hadi hapo watakapooneshwa soko la kudumu.
Mara kwa mara wafanyabiasahara wamekuwa wakiulalamikia Uongozi wa Manispaa ya Mpanda kwa kushindwa kuwatengea masoko ya kufanyia biasahara zao karibu na makazi yao wakisema kuwa wanashindwa kutekeleza Kauli mbiyu ya Hapa Kazi Tu ya Rais John Pombe Magufuli ili kujikwamua na umaskini.
Habarika Zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA