VIJANA UVCCM MKOANI KATAVI WAJITOKEZA KUCHANGIA DAMU SALAMA HOSIPTALI YA WILAYA YA MPANDA



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama –Mpanda Katavi
VIJANA WA UMOJA wa chama cha Mapinduzi UVCCM Mkoani Katavi,leo wamejitokeza kuchangia damu salama katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda.

Katibu wa umoja wa vijana UVCCM Mkoani Katavi Bw.Shua Masanguti amesema vijana wa chama hicho wapatao 80 wakiwemo wanawake 8 wamaejiotokeza kuchangia damu salama ili kunusuru maisha ya wagonjwa wanaolazimika kuongezewa damu.
Aidha Bw Masanguti amesema wamechukua hatua hiyo baada ya kutambua kuwa kuna uhitaji mkubwa wa damu kwa wagonjwa katika ikiwa pia ni sehemu ya kuadhimisha wiki ya vijana duniani ambayo kilele chake ni Oktoba 14 mwaka huu.
Mmoja wa wataalamu wa idara ya kitengo cha damu salama katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda Rinus Zenobi Kawana mbali nakuwapongeza  chama cha Mapinduzi CCM kwa uamuzi wa kutoa damu salama kwa ajili ya wagonjwa pia ametoa wito kwa makundi mengine kuendelea kujitokeza ili kuchangia damu.
Katika hatua nyingine Muuguzi Mkuu wa Manispaa ya Mpanda Dkt.Alexanda Gervas Kasagula  mbali na kuwapongeza vijana wa CCM kwa kujitokeza kuchangia damu salama amesema,ujenzi wa duka la kuhifadhiwa dawa linalojengwa na Bohari ya dawa hapa nchini MSD katika Hospitali ya Wilaya ya Mpanda limefikia hatua nzuri licha ya kuwa hata hivyo linaonekana kuwa dogo ukilinganisha na kiasi cha dawa kinachohitajika kuhifadhiwa katika duka hilo.
Ujenzi wa duka ni utekelezaji wa Agizo la Wziri Mkuu aliyeagiza kujengwa maduka ya madawa katika Hospitali zote hapa nchini ili kutatua tatizo la ukosefu au uhaba wa dawa kwa ajili ya wagonjwa.
Hospitali ya Wilaya ya Mpanda ambayo zamani ilikuwa ikimilikiwa na Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda kabla ya Manispaa ya Mpanda kukabidhiwa hospitali hiyo,bado ina uhaba wa damu kwa ajili ya wagonjwa wenye uhitaji wa kuongezewa damu.
Endelea kuhabarika na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri tuma kupitia p5tanzania@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA