TAASISI YA TWAWEZA WAENDESHA KONGAMANO LA WADAU WA ELIMU MPANDA,WAZAZI WALEZI WATAKIWA KUTAMBUA UMUHIMU WA ELIMU KWA WATOTO




Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
WAZAZI na WALEZI katika manispaa ya Mpanda Mkoani wameshauri jamii kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto ikiwa ni urithi kwa maisha bora.
Wanafunzi mkoani Katavi
                                               

Ushauri huo umetolewa leo katika kongamano la uwezo matokeo ya Elimu mwaka 2015, ambalo limewakutanisha wadau wa elimu kujadili utafiti wa Uwezo-Twaweza na jinsi ya kutatua matatizo ya elimu.
Akizungumza wakati akifungua kongamano hilo Mgeni rasmi ambaye ni Mdhibiti Ubora wa shule,Mpanda mjini,Hartson Kyejo amesema,elimu ya msingi ndiyo itakayomjengea uwezo mtoto kufanya vizuri maishani.
Wakizungumza katika kongamano hilo,wadau wa elimu wamebainisha baadhi ya matatizo yanayopelekea kudhorotesha elimu bora kwa wanafunzi wa shule za msingi kuwa ni pamoja na watoto kuwa walezi wa watoto wenzao katika familia, upungufu wa vyumba vya madarasa na utoro wa wanafunzi shuleni.
Kongamano hilo limeandaliwa na Uwezo-Twaweza kwa kushirikiana na Katavi Women Development Organization.
Katika Mkoa wa Katavi,Manispaa ya Mpanda ndiyo inayoongoza kwa namba moja kitaifa kwa miaka miwili mfululizo kwa kufaulisha mtihani wa darasa la saba ambapo ni mwaka 2014 na 2015 huku Mkoa wa Katavi kwa ujumla ukishika nafasi ya tatu kitaifa kwa kufaulisha wanafunzi.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri,tuma kupitia p5tanzania@gmail.com
 Mwandishi : Tizibazomo Bernard
Mhariri :Issack Gerald Bathromeo Mashama

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA