TANZANIA NA UHORANZI ZASAINIANA MKATABA WA KUWEKA UMEME WA UHAKIKA MKOANI KATAVI,ZAIDI YA VIJIJI 15 KUNUFAIKA



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Mpanda Katavi
SERIKALI za Tanzania na Uhoranzi kwa pamoja zimesainiana Mkataba wa Shilingi Bilioni 44/= ili kufanikisha ukamilika kwa mradi wa umeme wa uhakika Mkoani Katavi ifikapo mwezi Juni mwaka 2017.
Mashine zinazofua umeme
                                 

Hayo yamebainishwa na Meneja Taneco Mkoni Katavi Mhandisi Julius Sabu wakati akitoa taarifa ya hali ya umeme katika Mkoa wa Katavi kupitia kikao cha baraz ala madiwani.
Amesema kuwa katika kutatua matatizo ya kukosekana kwa umeme,Tanzania kwa kushirikiana na serikali ya Uhoranzi wamesainiana mkataba wa Shilingi Bilioni 44 ili kuweka  umeme wa uhakika Mkoani Katavi ambapo kila upande umechangia shilingi bilioni 22 kupitia mradi wa ORIAL.
Mhandisi Sabu pia amesema katika hatua ya awali jumla ya mashine 2 zinazozalisha umeme wa Kilowati 1200 sawa na Megawati 2.5 zinatarajiwa kufungwa ili kuzalisha umeme ni katika mradi huo wa ORIAL ambapo mpaka mradi utakapokamilika Mei 30 mwaka 2017 mashine 4 zinazotakiwa zitakuwa zimefungwa mashine 4.
Aidha amesema Mkandarasi wa Mradi wa ORIAL amekwishaanza kushughulika na mradi.
Katika mardi wa umeme wa ORIAL unatarajia kunufaisha vijiji 15 vya Mkoa wa Katavi ambavyo ni Magamba ,mtisi,Matandala ,Sitalike,kakese mbugani, Kalilankulukulu, Ifukutwa, majalila, Igalula,Kabungu,na shule ya Sekondari Mpanda.
Hata hivyo Kwa upande wake Shirika la umeme nchini Tanesco kwa sasa imetenga bajeti ya shilingi mil 350,888,669/= ili kupeleka umeme wa uhakika mara baad aya vifaa kuwasili Mkoani Katavi ambapo umeme huo utapelekwa katika maeneo ya Kasimba, misengeleni, Kazima, kilimahewa, Misunkumilo, Kichangani,Mpanda girls na Makanyagio.
Wakati huo huo Shirika la Tanesco baada ya kuwasilishwa kwa vifaa vya umeme hivi karibuni katika miradi mipya ambayo imepangwa,maeneo ya Kapalangao, Shanwe, Misengeleni, Misunkumilo,Nsemulwa,Kazima na Mpanda Hotel maeneo ya viwandani  ambayo imetengewa shilingi  milioni 525,769,846/=.
Mradi wa ORIAL hapa nchini unakuja kutekelezwa Mkoani Katvi baada ya kukamilika katika Wilaya za Ngara na Biharamulo zilizopo Mkoani Kagera
Hata hivyo  shirika la kuzalisha umeme hapa  nchini TANESCO mkoani Katavi limesema tatizo la kukatika kwa umeme mara kwa mara kutokana na uchakavu wa Mashine zinazozalisha umeme zilizopo.
Kwa sasa mashine zinazotumika  zilihamishwa kutoka Shinyanga na Njombe mwaka 1992 na 1994 ambapo mpaka sasa amshine zilizopo zimetumika kwa zaidi ya miaka 40.
Endelea kuhabarika zaidi na P5 TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Mawasiliano kwa ushauri : p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA