RPC KATAVI : JESHI LA POLISI LIMEJIANDAA KUWADHIBITI WAANDAMANAJI OPARESHENI UKUTA,VYAMA VILIVYOKUWA VIMEPANGA KUANDAMANA VYAAHIRISHA MAANDAMANO


Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
JESHI la Polisi Mkoani Katavi lilikuwa limesema limefanya maandalizi ya kutosha kuwadhibiti watu,kikundi au vyama vya siasa ambavyo vingefanya maandamano kesho Septemba mosi.
Viongozi wa upinzani wakati wa kikao na wanahabari Dar es Salaam
ACP Damasi Nyanda Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi(PICHA NA.Issack Gerald)Agosti 31,2016
                                          

Kauli hiyo ya onyo kwa watu na vyama vya siasa llilikuwa imetolewa leo na Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda,wakati akizungumza na vyombo vya habari Ofisini kwake.
Kamanda Nyanda alisema jeshi la Polisi limepiga marufuku kwa vyama vya siasa kufanya maandamano au mikutano mpaka pale maelekezo mengine yatakapotolewa.
Aidha alisema maandamaono au mikutano imepigwa marufuku kutokana na viashria vya uchochezi kwa wananchi dhidi ya serikali na kupelekea kusababisha uvunjifu wa amani.
Katika hatua nyingine Kamanda Nyanda amewataka wakazi Mkoani Katavi kutumia siku ya kesho ambayo ingetumika kwa maandamano wafanye shughuli za maendeleo.
Nao baadhi ya wananchi Mkoani Katavi wamesema watanzania wanatakiwa kujifunza madhara ya kufanya maandamano yanayotokea katika nchi nyingine zikiwemo Burundi na Lybia ambapo madhara makubwa ni kutokea kwa vifo na ulemavu wa kudumu.
Hata hivyo Muungano wa vyama vya upinzani nchini Tanzania kupitia mwenyekiti wa CHADEMA taifa Bw.Freeman Mbowe umeahirisha maandamano ya kitaifa ambayo yalikuwa yamepangiwa kufanyika kesho.
Viongozi wa upinzani,akiwemo Edward Lowassa wa Chadema, wametangaza hatua hiyo kwenye kikao mbele ya waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam.
Wamesema wameahirisha maandamano hayo kwa kipindi cha mwezi mmoja baada ya kusikia ombi la viongozi wa kidini na wadau wengine waliowaomba kukumbatia na kuyapa muda mazungumzo.
Miongoni mwa madai ya baadhi ya vyama vya siasa kikiwemo chama hicho kikuu cha upinzania CHADEMA ni Ukiukwaji wa utawala wa sheria unaofanywa na Serikali ya awamu ya 5 inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ambapo Maandamano hayo yaliyokuwa yamepangwa kufanyika yalikuwa yamepewa jina la Oparesheni Ukuta huku yalikuwa yamepangwa kuanza Septemba mosi bila Ukomo.
Kama kutashindikana maridhiano baina ya serikali na vyama hivyo vya siasa,maandamano hayo ymepangwa kufanyika tena Oktoba mosi mwaka huu.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA