RPC NYANDA KATAVI LEO KUZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI KUHUSU MAANDAMANO YA OPARESHENI UKUTA SEPTEMBA MOSI.



Na.Issack Gerald Bathromeo-Katavi
KAMANDA wa Jeshi la Polisi Mkoani Katavi ASP Damasi Nyanda leo anatarajia kukutana na waandishi wa habari Mkoani Katavi kuzungumzia mandamano ya Opareshen Ukuta yanayoratibiwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema.


Taarifa ya kamanda Nyanda ambayo imetolewa kwa waandishi wa habari na Afisa habari wa jeshi hilo Mkoani Katavi,mazungumzo hayo yanatarajia kufanyika kuanzia majira ya saa 3:00 asubuhi katika Ofisi ya Kamanda iliyopo makao makuu ya Jeshi la polisi Mkoa wa Katavi yaliyopo Kata ya Ilembo.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi mara kwa mara limekuwa likizungumza na waandishi wa habari ili kutoa taarifa kwa jamii kuhusu masuala mbalimbali yanayoendelea.
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi linatarajia kutoa tamko la katazo la maandamano ya Oparesheni Ukuta ikiwa ni siku moja baada ya Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika kutoa tahadhari kwa watakaofanya maandamano Septemba mosi mwaka huu ambao alisisitiza kuwa watakaoandamana jeshi la Polisi limejiandaa kuwadhibiti.
Habarika Zaidi na P5ANZANIA.BLOGSPOT

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA