WAKAZI WILAYANI TANGANYIKA WAAGIZWA KUONGEZA KASI YA KUJENGA SEKONDARI KILA KATA


Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama-Tanganyika
WAKAZI wilayani Tanganyika Mkoani Katavi kwa Kushirikiana na uongozi wa vijiji na kata  katika Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika,wameagizwa kuweka mikakati ya ujenzi wa shule za Sekondari kila kata ,ili kila mwanafunzi asome bila kuhangaika na badala yake apate elimu bora.
                                     
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Saleh Mbwana Mhando akishiriki ujenzi Shule ya sekondari ya Bulamata  kata ya Bulamata(PICHA NA Issack Gerald)Septemba 16,2016
                                        
Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika akizungumza na wananchi eneo la kijiji cha Busongola kunakojengwa Shule ya Sekondari Bulamata(PICHA NA.Issack Gerald) Septemba 16,2016
                                                     
Wananchi wa wanafunzi wa Shule ya Msingi Isubangala kijiji cha Isubangala kata ya Ilangu wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya(hayupo pichani)(PICHA NA.iSSACK gERALD) Septemba 16,2016

Agizo hilo limetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika Bw.Saleh Mbwana Mhando,wakati akizungumza na wananchi katika mikutano ya Hadhara ambayo ameifanya katika kata za Ilangu na Bulamata.
Aidha Mkuu wa Wilaya ametoa onyo kali kwa wazazi watakaohusika na kumuoza mtoto wa shule akisema kuwa sambamba na mwanaume atakayeoa au kumpa ujauzito mwanafunzi  watafungwa miaka 30 bila huruma.
Afisa Mtendaji wa Kata ya Bulamata Bw.Godfrey Mbalazi,akisoma taarifa ya ujenzi wa shule ya Sekondari ya Bulamata inayojengwa katika kijiji cah Busongola ,amesema kuwa ujenzi unaofanyika ni wa vyumba vitatu na ofisi moj aya walimu ambapo mpaka sasa wamekusanya zaodi ya shilingi milioni 12 kwa kuanza na ujenzi wa shule hiyo.
Kwa upande wake Mwakilishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Makazi Mishamo Bw.Harold Boserwe amesema kuwa,wao mpaka sasa wanasaidia magari kwa ajili ya kusomba maji ,matofali na mawe ili kuharakisha ujenzi ukamilike ambapo Mkuu wa Wilaya Bw.Mhando amesema kuwa inatakiwa wanafunzi waanze kusomea katika shule hiyo mwakani.
Halmshauri ya Wilaya ya Tanganyika ina kata 16 ambapo kati ya hizo kata 6 hazina Shule za Sekondari.
Wakati huo huo,Mkuu wa Wilaya akiwa katika Shule ya Msingi Isubangala iliyopokata ya Ilangu amezindua vyumba 3 vya madarasa na ofisi moja ambavyo vimefikia usawa wa renta katika ujenzi ambapo shule hiyo iliyoanzishwa 17.1.1980 mpaka sasa ina wanafunzi 1071.
Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya ameruhusu kufanyika mikutano ya viongozi wa vijiji na kata ilivyokuwa imezuiliwa na uongozi wa makazi ya mishamo kutokana na mgogoro wa kiutawala.
Katakika taarifa yake Afisa Mtendaji wa kata ya Ilangu Bw.Seuri Mishileki amesema,mikitano ilikuwa imezuiliwa kwa takribani wiki mbili mpaka sasa ambapo ameeleza  shughuli nyingi za maendeleo kukwama kutokana na kutokuwepo kwa mikutano inayowakutanisha viongozi na wananchi.
Chanzo cha Mvutano ni baada ya mwenyekiti wa kijiji cha Ilangu kujiudhuru na kuvutana kuwa anayechukua nafasi atoke makazi ya mishamo au upande mwingine.
Habari hii pia ipate kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni au ushauri au ukiwa na habari yoyote tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA