ASILIMIA 45 YA WATOTO CHINI YA MIAKA 18 TANZANIA HUPATA UJAUZITO NA KUPOTEZA MAISHA WAKATI WA KUJIFUNGUA



Na.Issack Gerald Bathromeo Mashama -Nkasi Rukwa
Asilimia 45 ya watoto wa kike waliochini ya  umri wa miaka 18 hupata ujauzito na kupoteza maisha kila mwaka  wakati wa kujifungua kwa mjibu wa  utafiti uliofanywa  na Shirika lisilokuwa la kiseriklai la Plan International Tanzania.

Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Uendeshaji wa   Shirika la Plan intenational Tanzania Gelard Magashi wakati wa zoezi la  uzinduzi wa mpango wa kuzuia ndoa za utotoni lililofanyika wilayani Nkasi Mkoani Rukwa  katika ukumbi wa St.Bakhita Chuo cha uuguzi Namanyere
Magashi  alieleza kuwa,zaidi ya watoto 16,000 elfu wapo katika ndoa za utotoni katika mikoa ya Morogoro,Rukwa na Shinyanga,hali ambayo imekuwa  ni tatizo kubwa ambalo limekuwepo katika jamii nyingi hapa nchini huku likionekana kutotiliwa maanani ikiwemo kutochukuliwa hatua madhubuti kwa wahusika.
Aidha alizungumzia changamoto kubwa iliyombele yao katika mapambano  ya kuzuia  mimba za utotoni kuwa ni pamoja na mila na desturi kwa baadhi ya makabilia hapa nchini,umasikini,uelewa na mtazamo finyu kwa jamii kuwa  mtoto wa kike ni kitegauchumi kwenye familia , 
Aidha alifafanua kuwa,mradi huo unatekelezwa katika wilaya ya kilombero mkoa wa morogoro na Nkasi wilayani Rukwa kuanzia mwaka huu wa 2016,hadi mwaka 2019 ambapo unalenga kufanya kampeni mbalimbali zitakazowezaesha kuondoa tabia za kuozesha watoto wadogo wenye chini ya umri wa miaka 18.
Kwa upande wake meneja wa mradi huo  wilaya ya Nkasi William Mtukananje  alisema ,plan international imejikita kuangalia maeneo mhimu ikiwemo Afya ya mama na mtoto,maji na usafi wa mazingira pamoja na  ulinzi na usalama wa mtoto ambapo wanatarajia kuanzisha mradi wa Afya katika wilaya ya nkasi ifikapo Januari 2017 ili kutoa huduma za kiafya kwa mama na mtoto kwa ukaribu na ufanisi zaidi.
Kwa upande wake Mgeni rasmi katika uzinduzi wa mradi huo Naye Vicent Magendela ambaye ni Afisa mtendaji mamlaka ya mji mdogo Namanyere kwa niaba ya mkuu wa wilaya ya Nkasi Said Mohammed Mtauda,alisema   shirika plan international Tanzani kwa ujio wao wilayani  ni  muhimu kutokana na  kuwa takwimu zinaonyesha aslimia 40% katika wilaya ya nkasi watoto wanaathiriwa na ndoa za utotoni.
Magendela alisema,serikali inafanya kila jitihada kuhakikisha miundombinu ya mama katika kujifungua  ikiwemo dawa hospitalini pamoja na mazingira ya kujifungulia yanaboreshwa ili kuepuka vifo vya mama na mtoto wakati wa kujifungua.
Mratibu wa plan international wilayani Nkasi Nestory Frank alitoa wito kwa wazazi na walezi kuwa, kila mmoja anawajibu katika kufanikisha malengo ya mradi huo, huku akiyataja baadhi ya  madhara ya ndoa za utotoni kuwa ni pamoja na watoto kunyanyasika kijinsia ,kiakili,kimwili pamoja na kuwa hatarini kupoteza maisha wakati wa kujifungua sababu ya kutokwa damu nyingi wakati wa kujifungua kwa kuwa viungo vyao vinakuwa bado havijawa tayari kuhimili kuzaa.
Kauli mbiyu ya Plan Itnernational Tanzania inasema ni “plan, watoto kwanza”.
Pata habari hii pia kupitia P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa Ushauri au maoni tuma kupitia p5tanzania@gmail.com

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA