NYUMBA ILIYOTEKETEA KWA MOTO JUZI ,CHUMBA CHA MPANGAJI HASARA NI ZAIDI YA MILIONI MOJA NA LAKI TANO(1,500,000).

Na.Issack Gerald Bathromeo-Mpanda
Imebainika kuwa janga la moto lililotokea juzi katika Mtaa wa Mpadeco Kata ya Mkananyagio Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi,umesababisha Bi.Grace Emmanuel Mkazi wa mtaa wa Mpadeco kata ya Makanyagio kupata hasara ya Zaidi ya Shilingi Miloni moja na laki tano (1,500,000).
B.Grace amesema Moto huo uliozuka mchana uliunguza Vitanda 2 vyenye thamani ya laki tano na elfu sitini(560,000),Magodoro mawili 5 kwa 6 yenye thamani ya Shilingi laki tatu(300,000),Maguni ya Mpunga 4 thamani yake zaidi ya Shilingi laki 2(200,000),Upotevu wa fedha taslimu Shilingi laki nne na nusu za mkopo zilizopotea wakati wa uokozi na nguo ambazo tahamani yake haijafahamika.
Akizungumza akiwa nyumbani kwake muda mfupi baada ya kutoka hospitali ya Wilaya ya Mpanda,alikolazwa baada ya kuzimia kutokana mshtuko alioupata baada ya kupata hasara hiyo,amesema kuwa hata hivyo hajatambua kiasi alichotumia kwa ajili ya matibabu.
Hata hivyo amekwishafungua jarada Polisi ili ili kufanya uchunguzi wa tukio hilo ambalo lilitokea muda mfupi baada ya kubadili mifumo ya mita kutoka bili kwenda mfumo wa Luku ambapo kwa mjibu wa mama aliyepata hasara Meneja wa Tanesco alisema kuwa huenda kulitokea hitilafu ndani ya nyumba.
Bi.Grace amesema anaishi na watoto wake 3,wadogo zake 6,mama yake 1 ambapo mume wake naye alikatiwa rufaa ya kwenda kutibiwa Bugando mwanza baada ya kuugua na hivyo kufanya idadi ya watu 10 wanaomtegemea yeye.
Kwa upande wake mmiliki wa nyumba hiyo ambayo alisema kuwa haina bima,alisema kuwa uchunguzi ufanyike ili haki itendeke ambapo mbali na kueleza kupata hasara ya kusuka upya mfumo wa umeme katika nyumba hiyo itakayopatikana,pia amewaomba wasamaria kujitokeza kumsaidia Bi.Grace kutokana na Hasara aliyoipata.
Hata hivyo jeshi la zimamoto na uokoaji Mkoani Katavi siku ya tukio walifika haraka mara baada ya kupata taarifa kupitia simu waliyopigiwa na kufanikiwa kuzima moto huo amabo kama wasingefika mpema nyumba nzima ingeungua na kusababisha hasara zaidi.
Hata hivyo serikali ya Kijiji kupitia kwa mwenyekiti wa serikali hiyo Bw.Bernad Nkana amesema kuwa mpaka sasa amekwishafikisha taarifa rasmi kwa kamati za majanga ngazi ya Tarafa na Wilaya ili kuangalia uwezekano wa kumsaidia Bi.Grace.
Mbali na Majang aya Moto katika mtaa wa Mpadeco,pia mtaa huo umekuwa ukikumbw ana majanga ya makazi ya watu kuezuliwa na mvua zinazoambatana na upepo ambapo mwaka jana,miongoni mwa waliopatwa na janga la mvua zilizoambatana na upepo ni Diwani wa kata ya Mpanda Hotel Mh.Liwali ambaye makazi yake yapo Mtaa wa Mpadeco.
Majanga mengine katika mtaa huo ni athari zitokanazo na mvua ambapo mawaka uliopita kuliripotiwa vifo vya watoto vilivyotokana na kusombwa na maji.
BI.GRACE EMAMMNUEL ANAOMBA MSAADA KUPITIA 0757 61 61 60.
Habarika zaidi na P5TANZANIA.BLOGSPOT.COM
Kwa maoni,ushauri au ukiwa na habari tutumie kupitia p5tanzania@gmail.com


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA