KINACHOIGUSA MIKOA YA KATAVI,RUKWA NA KIGOMA KUTOKA VIKAO VYA BUNGENI DODOMA LEO SEPTEMBA 8,2016

Na.Issack Gerald-Dodoma
Serikali imesema,inaendelea kuweka mikakati ya kuwa na kiwanda cha kutengeneza pikipiki za bodaboda ili kuwajengea vijana kuwa na uwezo wa kununua pikipiki zao,kuliko kuendelea kuwatumikia matajiri wenye uwezo wa kumiliki pikipiki hizo.
Wabunge wakiwa bungeni Mjini Dodoma leo Septemba 8,2016
                                  

Kauli hiyo imetolewa leo bungeni Dodoma na Naibu waziri mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki Mh.Suzan Kolimba wakati akijibu swali la Mh.Munde Tambwe mbunge viti maalumu Tabora aliyetaka kufahamu mikakati ya serikali kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kutengeneza pikipiki hapa nchini ukiwemo mkoa wa Tabora.
Mh.Tambwe amesema,ikiwa kiwanda cha Bodaboda kitajengwa Mkoani Tabora,vijana walio mikoa jiarani kama Katavi,Rukwa na Kigoma watanufaika kwa ukaribu zaidi.
Katika hatua nyingine Mh.Kolimba amesema,Wizara imekwishafanya mikakati ambapo na inaendelea v majadiliano na serikali ya chinayanaendelea kuhakikisha Serikali ya China inawekeza katika kilimo cha Tumbaku ili mku;lima wa Tanzania anufaike na zao la tumbaku.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA