RAIS MAGUFULI KUHUDHURIA SHEREHE ZA KUAPISHWA UHURU KENYATTA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.John Pombe Magufuli anatarajiwa kuungana na viongozi wa mataifa mbalimbali kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule Mh.Uhuru Kenyatta.

Taarifa ya serikali ambayo imetolewa na Mkurugenzi, Idara ya Habari-Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt.Hassan Abbasi imethibitisha hilo.

Mhe.Kenyatta anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumanne ya wiki ijayo jijini Nairobi ikiwa ni baada ya kushinda uchaguzi wa marudio uliofanyika Oktoba 26 mwaka huu nchini humo.

Rais Uhuru Kenyatta atakuwa anaongoza Jamhuri ya Kenya kwa kipindi cha awamu ya pili.


Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA