RAIS MAGUFULI ASISITIZA JENGO LA TANESCO KUBOMOLEWA

Na.Issack Gerald
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli amesisitiza kuwa jengo la TANESCO Ubungo ni lazima libomolewe kwa sababu yeye ndiye rais kwa sasa tofauti na zamani alipokuwa waziri.
Rais amesema hayo mapema leo wakati akihutubia wananchi ambao wamejitokeza katika ufunguzi wa Hospitali na Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) kampasi ya Mloganzila.
Aidha rais Magufuli amesema Jengo hilo lazima libomolewe hata nusu ya jengo iliyopoo katika hifadhi ya barabara huku akisema na kama ni kuondoa jengo lote basi inamaanisha kuwa pia jengo la wizara ya maji nalo itabidhi liondolewe kwa kuwa sheria ni msumeno.
Wakati huo huo rais amesema wakazi wa Kimara ambao nyumba zao zimebomolewa hawatalipwa fidia kwa sababu zilikuwa ndani ya hifadhi ya barabara na waliotakiwa kulipiwa fidia walikwishalipwa.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA