RC RUKWA APIGA MARUFUKU KUPAKIA MIZIGO KATIKA MWALO WA KIRANDO

SERIKALI mkuu mkoani  Rukwa imepiga marufuku  kuutumia mwalo uliopo katika  Kijiji cha Kirando ziwa Tanganyika kwa ajili ya kupakia na kushia mizigo kwani mwalo huo umetengwa kwa ajili ya shughuli za kuuzia samaki.
Mkuu wa mkoa huo Joachim Wangabo alisema hayo akiwa katika ziara ya kikai wilayani Nkasi na kukuta katika mwalo wa Kirando unatumika kama bandari ambapo malori yalikuwa yakipakua na kupakia mizigo kwa lengo la kusafisirisha  kuipeleka kwenye visiwa vilivyopo ziwa Tanganyika.
Alisema kuwa wananchi wasipotoshe lengo la kutebnwa kwa  mwalo huo ambayo ni kwaajili ya kuuza na kununua samaki wavuliwao kwenye ziwa Tanganyika na si  kwaajili ya magari kupakilia mizigo.
Mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa sehemu iliyotengwa ikitumika kama bandari haiko vizuri basi waone namna ya kuboresha ili sehemu hiyo ilirudi kama ilivyokuwa na sio kuikimbia na kuiacha kama ilivyo jwani kukimbia tatizo sio suluhisho bali kupambana na changamoto zilizopo na kuboresha.
Awali kabla ya Kukaribishwa Mkuu wa Mkoa, Mbunge wa Nkasi Kaskazini Ali Kessy alikemea vitendo vya wananchi wa Kirando kutumia mwalo huo kama bandari jambo ambalo ni kinyume na sheria na kuwataka kuacha tabia hiyo mara moja.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Said Mtanda aliwaasa wananchi wanaotumia vyombo usafiri ziwani kuzingatia kuvaa maboya na kuonya kutozidisha mizigo na abiria na kuwasisitiza wasafiri wa majini kuwa watumiaji wawe wantoa taarifa endapo wataona taratibu zinakiukwa kwakuwa wasafirishaji hao huangalia faida kuliko usalama wa maisha ya abiria wao.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA