WAFANYABIASHARA WILAYANI MPANDA WASITISHA MGOMO WA SIKU MBILI

Mamia ya wafanyabiasahara katika masoko ya Mpanda Mkoani Katavi leo wameanza kufanya biashara kama kawaida kufuatia kuwepo kwa mgomo huo kwa muda wa siku mbili.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti wamesema wamefanya mazungumzo na uongonzi wa Chama cha Mapinduzi CCM mkoani Katavi ili kufikia mwafaka wa mgomo uliosababishwa na kupandishwa kwa bei ya Pango kutoka sh 15,000 kwa hapo awali na kufikia shilingi 60,000.
Kwa upande wa Mwenyekiti wa Soko la Buzogwe ambalo ni kitovu cha mvutano huo Bw.Ramadhani Karata  amedai amekuwa  mafichoni  kwa muda kutokana na kuandamwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za yeye kuwa chanzo.
Mgomo wa wafanyabiashara hasa katika soko kuu la Wilaya ya Mpanda na Soko la Buzogwe ulianza juzi ambapo Mkuu wa Wilaya alikuwa amesisitiza kuwa mfanyabiashara asiyetaka kulipa tozo hizo arudishe chumba cha biashara.
Hata hivyo mwafaka kamili kuhusu kiasi ambacho kinatakiwa kulipwa na wafanyabiashara kinatarajiwa kutolewa baada ya wiki moja hiyo ikiwa ni kwa mjibu wa maazimio yaliyoafikiwa katika mkutano ulioendeshwa na Chama cha CCM Mkoani Katavi.

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA