WAZIRI WA MAJI ISACK KAMWELWE ATEMBELEA BWAWA LA IGOMBE TABORA ASISITIZA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Waziri wa Maji na Umwagiliaji,Mhandisi ISACK KAMWELWE amewataka wananchi Mkoani Tabora kutoharibu mazingira ya bwawa la Igombe ambalo kwa sasa limejaa ili kuzuia upotevu wa maji unaosababisha kero ya mgao wa maji.
Waziri Kamwelwe ambaye pia ni mbunge wa Jimbo la Katavi Mkoani Katavi,ametoa rai hiyo alipotembelea bwawa la Igombe kukagua hali ya ujazo wa maji ambapo amesema wananchi wamekuwa wakilima pembezoni mwa bwawa hilo na kusababisha upotevu wa maji hivyo ni vyema wakaacha utamaduni huo.
Amesema ili kuhakikisha wakazi wa Tabora wanaendelea kupata maji,serikali inaendelea kutekeleza mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria ambapo kwa sasa tayari mabomba ya kupitishia maji tayari yameanza kufika.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira mjini Tabora-Tuwasa Mhandisi Mkama Bwire amesema ujazo wa maji katika bwawa la Igombe umeongezeka kutoka mita moja mwaka jana hadi kufikia mita 4.6 kwa sasa hali ambayo imeondoa adha ya mgao wa maji.
Naye Mkuu wa wilaya ya Tabora,Mwalimu Queen Mlozi amempongeza Waziri Kamwelwe kwa juhudi zake za kuhakikisha changamoto ya mgao wa maji inaondoka kwa wakazi wa Tabora.
Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Tuwasa,Mhandisi Mkama Bwire mwaka jana mamlaka hiyo ilikuwa ikitumia zaidi ya shilingi milioni 200 kila mwezi kutibu maji lakini kwa sasa kiwango hicho kimepungua hadi kufikia milioni 180 na kinatarajia kupungua zaidi.
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA