WAWILI WAUWAWA KATIKA MAJIBIZANO YA RISASI KATAVI

Na.Issack Gerald
Jeshi la Polisi Mkoani Katavi limewauwa watu wawili kati ya watano waliokuwa na silaha tatu za kivita aina ya SMG ambapo watu hao wameuawa wakati wa majibizano kati yao na Jeshi la Polisi.
Kamanda wa Polisi Mkoani Katavi ACP Damasi Nyanda amesema tukio hilo limetokea Januari 25 mwaka huu katika kijiji cha Kapalamsenga Wilayani Tanganyika ambapo watu hao wamekutwa wakiwa na risasi 16 na Magazini 5.
Aidha Kamanda Nyanda amesema watu hao wamekutwa na meno ya Tembo yenye uzito wa kilo 6.6 yakiwa na thamani ya zaidi ya Shilingi milioni 34  pamoja na nyama ya pofu kilo 20 yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 3
Kwa upande wake Mkuu wa Hifadhi ya taifa ya Katavi Zumbe Msindai amesema kukamatwa kwa watu hao kumetokana na ushirikiano kati yao na jeshi Polisi Mkoani Katavi ikiwa ni baada ya kupata taarifa za siri juu ya uwepo wa watu hao.
Watuhumiwa wote wanatarajiwa kufikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika

Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA