ALIYEKUWA MKURUGENZI WA TBC AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KUTAPANYA SHILINGI MIL. 897


Aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania TBC, Tido Mhando amefikishwa mahakamani jijini Dar es Salaam kwa mashtaka ya matumizi mabaya ya Madaraka.
Tido Mhando
Tido Mhando,ambaye kwa sasa ni Mkurugenzi wa Azam Media alifikishwa katika mahakama ya Kisutu mapema jana Ijumaa na kusomewa dhidi mashtaka yake.
Wakili wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Tanzania (Takukuru) Leonard Swai alimwaambia hakimu mkazi mkuu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Victoria Nongwa kuwa Mhando anatuhumiwa kwa mashtaka matano.
Bw.Mhando anadaiwa kutenda makosa hayo mwaka 2008 alipokuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC na anatuhumiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka wakati alipokuwa akilitumikia shirika hilo la Utangazaji la Serikali TBC ambapo anadaiwa kulitia hasara taifa shilingi milioni 897.
Hata hivyo Mhando amekana mashtaka yote na kuachiwa kwa dhamana ambapo kesi imeahirishwa hadi Februari 23mwaka huu kwa ajili ya kusomewa maelezo ya awali.
Sheria nchini Tanzania haiwaruhusu washtakiwa,mawakili au watu wengine kuzungumzia kesi nje ya mahakama.
Mhando ni miongoni mwa waandishi wa habari na watangazaji wakongwe wa Tanzania na aliwahi kufanya kazi Shirika la Utangazaji Uingereza (BBC) kama Mkuu wa Idhaa ya Kiswahili kabla ya kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TBC.
Pia amewahi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited (MCL) inayochapisha magazeti ya Mwananchi,Mwanspoti na The Citizen.
Katika hatua nyingine aliwahi kufanyia kazi Sauti ya Ujerumani (Deutsche Welle),Sauti ya Amerika na Shirika la Utangazaji la Kenya (KBC) lilipokuwa linafahamika kama Sauti ya Kenya (VoK).
Chanzo:bbc
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA