HAKIMU ATAKA WATENDAJI WA MAHAKAMA WAWAJIBIKE KWA MJIBU WA SHERIA

Hakimu mfawidhi wa mahakama ya mkoa wa Katavi Hassan Omary amewataka watendaji wa mahakama kusimamia maadili ya kazi zao katika uwajibikaji wa kuwatumikia wananchi katika kutoa maamuzi mbalimbali ya kesi wanazoziendesha ktika maeneo yao yakazi.
Bw.Omary amesema kuna baadhi ya malalamiko ambayo amekuwa akiyapokea kutoka kwa wananchi yanayowalenga moja kwa moja baadhi ya watumishi wa mahakama katika utekelezaji wa majukumu yao kwa wananchi hasa yale ya ucheleweshwaji wa maauzi ya kesi pasipo na sababu za msingi
Aidha amesisitiza kuwa nivyema wanachi kufahamu kuwa mahakama ndiyo sehemu sahihi ya kukimbilia pindi wanapoona haki zao zinapolwa na watu wasio jua taratibu kanuni na sheria za nchi pamoja na hayo amesema muhimili huo wa utoaji haki nivyema ukaachwa ufanyekazi yake pasipokuingiliwa na Mtu au taasisi yeyote katika utoaji wa maamuzi mbalimbali ya kesi
Kwa upande wake afisa Tehama wa mahakama hiyo Bw.James Kapele amesma kuwepo kwa mfumo wa kieletroniki katika undeshaji wa kesi mbalimbali kumepunguza mlundikano wa kesi ambao ulikuwa unajitokeza kabla ya mfumo huo wa kuanza kutumika hapanchini
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA