RAIS MAGUFULI,KENYATTA,NKURUNZIZA,IDRISI,MAHAKAMA YA KENYA NA JSEHI LA ZIMBABWE WATUNUKIWA TUZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli ametunukiwa tuzo ya amani ya Mandela (Mandela Peace Prize) kwa kuendeleza shughuli ya kulinda amani na kupigania usawa wa kijamii.
Rais Magufuli mwenye miwani katika picha
Marais wengine ambao wamepata tuzo ni Rais Uhuru Kenyatta ambaye amejishindia tuzo ya Mandela ya Demokrasia kutokana na kuendeleza demokrasia nchini Kenya.
Mahakama ya Juu nchini Kenya na Jeshi la Zimbabwe zimetunukiwa tuzo ya ujasiri (Mandela Boldness) kwa kufanya uamuzi kwa kijasiri kwa masilahi ya mataifa yao.
Rais wa Taasisi ya Mandela,Dk Paul Kananura amesema Rais Kenyatta ametunukiwa kwa kudhihirisha demokrasia kwa kukubali uamuzi wa Mahakama ya Juu hivyo kuheshimu kanuni za utengano wa mamlaka.
Mahakama ya Juu ya Kenya ilibatilisha matokeo ya urais katika uchaguzi wa Agosti 8,2017 yaliyompa ushindi Kenyatta na kuamuru uchaguzi kurudiwa ambao alishiriki na kuibuka mshindi.
Rais wa Chad, Idriss Itno amepata tuzo ya Mandela ya Ulinzi (Mandela Security) kutokana na sera ya kupambana na ugaidi katika maeneo ya Sahel na Ziwa Chad. Rais wa Burundi, Pierre Nkurunziza akituzwa tuzo ya ujasiri (Mandela Courage).
Chanzo:Mwananchi
Habari zaidi ni P5TANZANIA LIMITED


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA