JAJI MKUU WA TANZANIA ATOA WARAKA MZITO KWA MAHAKAMA MKOANI KATAVI


Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Khamisi Juma ametoa waraka kwa Mahakama ya hakimu mkazi  Mkoa wa Katavi unaokataza Tozo ya malipo kwa hati za  hukumu ambazo ilikuwa inatozwa kwa wananchi .
Jaji mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Khamisi Juma
Kwa mjibu wa Afisa mawasiliano na Tehama wa mahakama hiyo Jemes Vedasi Kapele amesema waraka huo unaelekeza usitishwaji wa tozo za hati za hukumu.
Aidha Afisa huyo  amesema kufutwa kwa tozo hizo kutakuwa mkombozi kwa wananchi wengi wenye kipato cha chini kwani walikuwa wakishindwa kumudu gharama zinazotakiwa kutokana na ukosefu wa fedha wanapohitaji kuapitwa haki zao kwa mjibu wa sheria.
Mara kadhaa baadhi ya wananchi wamekuwa wakionekana kutumia baadhi ya aseti kama ardhi ili kugharimia gharama zinazohitajika.
Jaji mkuu ametoa waraka huo ikiwa ni siku chache zimepita baada ya kufanya ziara mkoani Katavi na kutoa kauli ya kufuta tozo hizo.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA