MIL.40 KUOKOA WANAFUNZI SHULE YA MSINGI IGALULA WANAOSOMEA NJE WILAYANI MPANDA

Wanafunzi Shule ya Msibgi Igalula chini ya Mti wakitumia mti huo kama darasa

Juma Khatibu Chum akizindua vyumba vya madarasa Shule ya Msini Igalula ilyopo Wilayani Mpanda

Wanafunzi wa Chekechea Igalula Wilayani Mpanda wakiwa darasani

NA.Theressia Lwanji- Katavi
Ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi Igalula unatarajia kupunguza adha ya uhaba wa madarasa katika shule hiyo na kuondoa adha hiyo inayowapata wanafunzi shuleni hapo.

Kujengwa kwa madarasa hayo kunapunguza idadi ya vyumba vya madarasa kwa shule za msingi wilayani mpanda mkoani katavi.
Akisoma taarifa ya ujenzi wa vyumba hivyo kwa kiongonzi wa mbio za mwenge kitaifa mwalimu wa shule hiyo Brown Jasson amesema ujenzi huo utakuwa na manufaa kwa wananchi  kuwapeleka watoto shule ili kupata haki yao ya msingi.
Amesema halmashauri imewashirikisha wananchi katika ujenzi huo ili kutekeleza ilani ya serikali ya kuwashirikisha wananachi ili kutambua kuwa miradi ni yao.
Aidha amesema mradi huo umegharimu shilingi milioni arobaini na nne  mia tisa elfu ambazo ni mchango wa halmashauri,shilingi milioni therathini mia nne elfu kutoka kwa wahisani, milioni kumi na moja kutoka chama cha msingi cha tumbaku na nguvu za wananchi zikipatikana milioni tatu na laki tano.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA