NSIMBO YAANZA MAANDALIZI SIKUKUU ZA NANENANE KITAIFA,UWANJA UTAKAOTUMIA WAWA CHANGAMOTO

Na.Issack Gerald-Nsimbo,Katavi

Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi imeanza maandalizi ya sikukuu ya Wakulima nane nane huku ikikabiliwa na changamoto ya uwanja kwa ajili ya maadhimisho hayo.


Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bw. Michael Nzyungu amesema hayo wakati akizungumza na Mpanda Radio Ofisini kwake.

Amesema Nsimbo inatarajia kuadhimisha sherehe za nanenane mwezi ujao mwaka huu kufuatia waratibu wa sherehe hiyo kikanda ngazi ya taifa kuwataka kufanya hivyo.

Aidha amesema kuwa ili sherehe zifanyike kwa ufanisi, inahitajika fedha ya kutosha ambapo suala hilo limewasilishwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa ili kufanikisha shughuli hiyo.

Sikukuu ya wakulima nanenane huadhimishwa kila mwaka Agosti nane ambapo maadhimisho hayo kitaifa mwaka jana yalifanyika Mkoani Lindi.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA