WALEMAVU MPANDA WAOMBA MAADHIMISHO KUFANYIKA NGAZI YA HALMASHAURI






NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi
Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imesema inasubiri mwongozo wa serikali kuu ya Mkoa wa Katavi ili kuona kama kuna uwezekano wa kuandaa maadhimisho siku ya walemavu duniani mwaka huu.
Hayo yamebainishwa leo na Mkurugenzi Mtendaji Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda Estomihn Chang’a wakati akizungumza na mtandao huu Ofisini kwake.

Ufafanuzi huo wa Mkurugenzi Chang’a unakuja baada ya viongozi wa vyama vya walemavu Mkoani Katavi kuwasilisha barua kwa Mkurugenzi wakiomba maadhimisho kufanyika ngazi ya Halmshauri wakati yanapokuwa yakifanyika kitaifa katika mikoa mingine.

Kwa mjibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Walemavu wasioona Mkoani Katavi Issack Mlela hivi karibuni amesema,maadhimisho haya yanayofanyika Oktoba kila mwaka yatafanyika mwezi Novemba mwaka huu Mkoani Tabora baada ya kupisha Uchaguzi Mkuu mwezi Oktoba hapa nchini.

Maadhimisho haya yalifanyika mwaka jana Mkoani Dodoma baada ya kuahirishwa kufanyika Mkoani Tabora kutokana na Mkoa wa Dodoma kuwa nyuma katika kushughulikia masuala yanayohusu walemavu.






Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA