RAIS KIKWETE AVUNJA BUNGE,AELEZA MAFANIKIO NA CHANGAMOTO KIPINDI CHA UONGOZI WAKE






Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania hii leo amehutubia rasmi bunge la 10 la nchi hiyo na kulivunja rasmi.
Rais Kikwete ametumia nafasi hiyo kuainisha changamoto na mafanikio mbali mbali yaliyofikiwa katika uongozi wake wa miaka 10 madarakani kabla ya kuagana na wabunge hao.
Pamoja na mambo mengine, Bunge hilo litakumbukwa kwa mjadala mkali uliohusu maamuzi ya sakata ya uchotwaji wa zaidi ya shilingi bilioni 200 za akaunti ya Tegeta Escrow iliyokuwa benki kuu ya Tanzania.
Sakata hiyo liliwaondoa mawaziri wawili na katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini na vigogo wengine wa Ikulu ya rais.
Hata hivyo hotuba yake imesusiwa na idadi kubwa ya wabunge wa upinzani baada ya kulisusia bunge hilo kwa madai ya kupitisha miswada kadhaa bila kufuata utaratibu amabapo pia wabunge kususia mikutano lilifanyika mwaka 2010 wakati Kikwete alipokuwa akilifungua bunge la kumi.

Hivi karibuni Wabunge wa upinzani walitangaza kususia vikao vya mwisho vya Bunge hilo kutokana na uamuzi wa serikali kuwasilisha miswaada mitatu ya mafuta na gesi kwa hati ya dharura hali iliyopelekea Spika wa Bunge Anna Makinda kuahirisha bunge kwa muda usiojulikana ambapo hata hivyo aliwasimamisha baadhi ya wabunge kushiriki baadhi ya vikao kwa mjibu wa kanuni za bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA