WAWILI WAFIKISHWA MAHAKAMA YA WILAYA MPANDA KWA VITENDO VYA RUSHWA



Na.Theressia Lwanji-Mpanda Katavi
WATU Wawili wamefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Mpanda kwa kosa la  Kujihusisha na Vitendo Vya kutoa na Kupokea Rushwa Kinyume cha Sheria.


AKizungumza namtandao huu Naibu Mkuu wa Taasisi ya Kupambana na Rushwa Mkoani Katavi CHRISTOPHER NAKUA amesema Kwa Kipindi cha Kuanzia Mwezi January Mpaka June Mwaka huu Takukuru imewafikisha watu wawili Mahakamani huku Kesi nyigine zikiendelea Kuchunguzwa.

Katika hatua nyingine NAKUA ameitaka jamii kushirikiana na Takukuru kwa kutoa taarifa za Watu wanaojihusisha na Vitendo vya Rushwa kwa Vyombo vya Usalama ili Sheria ichukuliwe dhidi yao.

Hata hivyo takukuru imekuwa ikishauliwa na wadau wa masuala mbalimbali ya kijamii kuwa makini kufuatilia matukio yanayopekea kuwepo kwa vitendo vya rushwa Mkoani Katavi hususasni kipindi cha uchaguzi ujao wa udiwani,ubunge na urais.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA