WALAZIMIKA KULA VYAKULA WAKIWA NDANI YA NETI WAKIWAKIMBIA NZI

Moja ya madampo ya taka yanayotoa taka Mpanda mtaa wa Kashaulili

NA.Meshack Ngumba-Katavi
WAKAZI wa Mtaa wa Kashaulili  Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi hulazimika Kula chakula wakiwa ndani ya Neti kutokana na eneo hilo kuwa na inzi wengi.

Wakizungumza na Mpanda Fm wakazi wa eneo hilo wamesema wanajifunika neti kutokana na kuwepo kwa Inzi wengi wanaosabishwa na Jalala la Uchafu lililopo Katikati ya Makazi yao.
Wakazi hao wameongeza  kuwa Pamoja na Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Kufika eneo hilo na Kuagiza Kuondolewa kwa Jalala hilo bado uongozi wa Manispaa ya Mpanda Umeshindwa Kutekeleza agizo lake.
Ni hivi Karibuni iliyokuwa halmashauri ya Mji wa Mpanda na sasa Manispaa ilitangazwa kuwa halmashauri ya Kwanza Nchini inayozingatia Usafi wa Mazingira.
Hata hivyo licha ya Mkuu wa Moa wa Katavi Dr.Ibrahim Msengi kwa kushirikiana na viongozi mbalimbali waliopo katika Halmshauri nne za wilaya kuhamasisha usafi,bado wakazi wa baadhi ya maeneo hususani Manispaa ya Mpanda wanalalamika kuzagaa kwa takataka katika makazi yanayowazunguka licha ya kuambiwa kuwa gari la kuzoa taka hizo lipo ili hali taka hazizolewi.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA