JARIBIO LA KUUA KWA IMANI ZA USHIRIKINA WATU SITA WASHIKILIWA


 Na.Issack Gerald-Katavi
Watu sita wanashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani Katavi kwa tuhuma za kutaka kuvamia na kufanya mauaji ya watu wanaodhaniwa kuwa ni wachawi.

Kamanda wa polisi Mkoani Katavi Dhahiri Kidavashari amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuwa limetokea usiku wa kuamkia jana katika kijiji cha Ikola kata ya Ikola tarafa ya Karema Wilayani Mpanda.
Kidavashari amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na jeshi la wananchi kituo cha Ikola limefanikiwa kuzima jaribio hilo la mauaji na kuchoma moto kituo cha polisi kwa tuhuma za kuwa mwenyekiti wa kijiji cha Mpalamawe B kukataa kutajwa kwa wanadhaniwa kuwa wachawi hadharani.
Aidha ametoa wito kwa jamii kuacha kujichukulia sheria mkononi na badala yake kutoa taarifa katika vyombo vya usalama.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA