MKUU WA MKOA WA KATAVI AFUTURISHA,MAMIA KADA MBALIMBALI ALIOWAARIKA WAHUDHURIA AWAASA KUDUMISHA AMANI

Mkuu wa Mkoa akizungumza na kada mbalimbali aliowaarika kushiriki kwa pamoja katika Ikulu ndogo Mjini Mpanda

Mkuu wa Mkoa katikakti wakifuturu

Mkuu wa Mkoa wa Katavi wa NNE kutoka kulia katika picha wakiswali 

Na.Issack Gerald-Katavi
MKUU wa Mkoa wa Katavi Dk. Ibrahim Hamisi Msengi amesisitiza kuwepo kwa amani, upendo na ushirikiano na kusema kuwa  ni fursa nzuri kwa watu kufanya shughuli za maendeleo.

Dk. Msengi ametoa kauli hiyo jana katika hafla fupi ya kufuturisha iliyofanyika Ikulu ndogo mjini Mpanda.
Aidha amewataka wakazi wa mkoa wa Katavi kuondoa tofauti za itikadi za kidini na kisiasa na badala yake amewataka kudumisha amani.
Amesema kuwa kuepukana na vitendo viovu kutadumisha umoja wa watanzania kama ilivyo sasa ambapo Watanzania wote ni wamoja na wanashirikiana kwa kila jambo. 
Akizungumzia dalili za uovu,Mkuu huyo wa Mkoa amewataka wakazi wote mkoani Katavi kutoa taarifa kwa vyombo vya dola pindi wanapoona kuna dalili zozote za uvunjifu wa amani ili hatua za haraka zichukuliwe.
Hafla hiyo fupi ya futari, ilihudhuriwa na viongozi wa dini wakiongozwa na askofu wa kanisa la New harvest Afrika mashariki na kati Askofu Laban Ndimubenya, viongozi wa serikali, waumini wa dini mbali mbali na waandishi wa habari.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA