SAKATA LA WATU KULA VYAKULA WAKIWA KWENYE VYANDARUA,MKURUGENZI MANISPAA YA MPANDA ANG'AKA WAKAZI KUTUPA TAKA SEHEMU ZILIZOZUIWA


Na.Issack Gerald-Katavi
Mkurugenzi wa Manispaa ya Mpanda Suleiman Lukanga amesema eneo linalolalamikiwa na wakazi wa Mtaa wa Kashaulili kutumika kama Dampo la kutupa taka na kusababisha Nzi kuzagaa katika makazi yao lilishapigwa marufuku.

Mkurugenzi huyo anasema hayo  leo wakati akizungmza na P5 TANZANIA ikiwa ni siku mbili baada ya wakazi wa Mtaa wa Kashaulili kusema kuwa wanalazimika kula chakula wakiwa ndani ya vyandarua kujikinga na nzi wanaozagaa na kuangukia katika vykula wanapokuwa wanakula.
Aidha Mkurugenzi amesema ikiwa kamati zinazohusika na usafi katika mtaa huo hazifanyi kazi za kudhibiti utupaji taka katika eneo hilo watawajibishwa kwa mjibu wa sheria.
Pia amesisitiza kuchukuliwa hatua za kisheria kwa wakazi wanaotupa taka katika eneo lililozuiwa.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA