MWENYEKITI WA MTAA MANISPAA YA MPANDA AZUSHIWA KUJIDHURU,MTUHUMIWA AKANA KUHUSIKA


 NA.Issack Gerald-Katavi
Mwenyekiti wa Mtaa wa Kachoma uliopo Manispaa ya Mpanda Mkoani Katavi Mwarabu Kestokecha amewalalamimkia baadhi ya watu akiwemo aliyekuwa diwani wa kata ya Makanyagio katika Manispaa hiyo Iddi Nziguye kwa kusambaza taarifa za kupotosha wananchi kuwa amejiudhuru uenyekiti wa mtaa huo.

Akizungumza leo na P5 TANZANIA,Kestokecha amesema anasikitishwa kwa uvumi huo unaolenga kuchafua sifa zake za uongozi.
Kestokecha ambaye ni mwenyekiti kupitia chama cha CHADEMA amewataka wakazi anaowaongoza kutofuata maneno yasemwqayo mitaani na kusema kuwa anatambua thamani ya kura yao hivyo hawezi kutupa thamani ya kura waliyompa.
P5 TANZANIA imemtafuta mmoja wa watuhumiwa Idd Nziguye ambaye hata hiyo amekana kuhusika na usambazaji wa uvumi huo wa mwenyekiti huyo kujidhuru.
Mwarabu na Nziguye wote walilkuwa chama kimoja cha Chadema isipokuwa Nziguye inasemekana amehamia Chama kipya cha ACT Wazalendo kilichopo chini ya kiongozi Zitto Zubery Kabwe

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA