BALAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA WILAYA YA NSIMBO MKOANI KATAVI LAVUNJWA





 Na.Issack Gerald-Nsimbo,Katavi
BARAZA la Madiwani Katika halmashauri ya Nsimbo Mkoani Katavi  limevunjwa jana kwa Mjibu wa kanuni za baraza hilo ambalo humaliza muda wake wa kuwa  madarakani Kila baada ya Kipindi cha Miaka mitano.

AKizungumza katika kikao cha mwisho cha baraza hilo mwenyekiti wa halmashauri ya Nsimbo Mohamed Asenga  amesema kwa kipindi cha Miaka mitano Madiwani kwa kushirikiana na watalaam wamefanya kazi kubwa ya Kuleta maendeleo Katika jamii licha ya Halmashauri ya Nsimbo kuwa changa.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mlele Kanali ISSA SULEIMAN NJIKU mbali na kutoa pongezi kwa madiwani wote kwa kufanikisha shughuli za maendeleo kwa kipindi cha miaka mitano,amewataka madiwani watakaochaguliwa katika Uchaguzi Ujao wa urais ubunge na udiwani kuendeleza Ushirikiano wa kuleta maendeleo ya wananchi.

Halmashauri ya Wilaya nsimbo imetokana  na  Halmashauri ya Mpanda vijijini, ambapo  imevunja baraza la madiwani  kwa mara ya kwanza ikiwa na madiwani kumi na nne.

Miongoni mwa miradi ya maendeleo ambayo imeshughulikwa katika kipindi cha miaka mitano ni miradi ya maji,ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Wilaya na ujenzi wa maambara katika shule za sekondari.

Halmashauri hii ni miongoni mwa halmshauri nne zilizopo Mkoani Katavi ambazo ni Halmashauri za Mpanda Mji,Mpanda Vijijini,Nsimbo na Mlele.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA