USALAMA KAMBI YA WAKIMBIZI KATUMBA RAIA WAPYA TANZANIA YAENDELEA KUIMARIKA



Na.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
HALI YA USALAMA imeendelea  kuimarishwa zaidi katika kambi ya wakimbizi ya Katumba iliyopo Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi.

Hayo yameelezwa leo na Inspector Msaidizi wa Polisi katika kambi hiyo  NDITA MALE Katika mahoijiano na  mwaandishi wa habari wa blogi hii katika kambi hiyo.
Katika hatua nyingine Insipecta Male amekanusha taarifa za Uvumi wa kuwa jamii ya Watanzania wapya wanajihusisha na Vitendo vya Uhalifu katika maeneo mbalimbali Mkoani Katavi  na kuongeza kuwa Uhalifu uliokuwa ukijitokeza kipindi cha Nyuma kwa sasa umedhibitiwa.
Kufuatia kuwepo kwa taarifa hizo wakazi  Katika kambi hiyo wametakiwa kuachana na Vitendo vya uhalifu wa aina yoyote ili kuepuka Mkono wa Sheria.
Zoezi la kutoa vyeti vya uraia   kwa wakimbizi  walioishi zaidi ya miaka arobaini nchini Tanzania wengi wao wakitokea nchini Burundi lilifanyika mwaka jana ambapo wakimbizi zaidi ya laki moja walipewa uraia.
Mkoa wa Katavi una makambi mawili ya wakimbizi ambayo ni Katumba yenyewe iliyopo halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo na Kambi ya mishambo iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA