WAZIRI MKUU PINDA AKATAA KUGOMBEA UBUNGE JIMBO LA KATAVI,AWAACHIA WENGINE KUCHUKUA JIMBO HILO



Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda

NA.Issack Gerald-Mlele Katavi
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amekataa ombi la wananchi wa jimbo lake la uchaguzi la kumtaka agombee tena ubunge katika jimbo hilo ili kuendeleza mipango mbalimbali ya maendeleo aliyoianzisha.

Akizungumza baada ya Ibada ya Jumapili katika kigango cha Kanisa Katoliki cha Kibaoni wilayani Mlele,Waziri Mkuu Pinda amesema anamshukuru Mungu kwa nafasi aliyopewa ya kulitumikia Taifa akiwa Waziri Mkuu kwa miaka minane na anaamini wakati umefika wa yeye kuwaachia wengine nafasi ya ubunge wa jimbo la Katavi.
Waziri Mkuu Pinda Amesema,ataendelea kuwa karibu na wananchi wa Katavi wakati wote na kwa vile atakuwa na muda wa kutosha atashiriki kikamilifu katika mikakati mbalimbali ya kuwaletea maendeleo wananchi ili waweze kujikwamua kutoka kwenye umaskini.
Waziri Mkuu yuko kijijini kwake Kibaoni, wilayani Mlele kwa ajili ya mapumziko mafupi.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda alikuwa miongoni mwa makada 42 wa CCM waliokuwa wametangaza kugombea urais wa Tanzania Kupitia Chama cha Mapinduzi ikiwa angeteuliwa na chama chake ambapo hata hivyo John Pombe Magufuli mbunge wa Chato Mkoani Geita alipitishwa na chama hicho kuingia kinyang’anyiro cha urais Oktoba 25 mwaka 2015.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA