MPANDA GIZA NENE SUAL LA UMEME,TANESCO YASEMA UMEME KUTENGAMAA MIEZI MITATU IJAYO


 
Mafundi wakiwa katika matengenezo ya mitambo ya Tanesco Mpanda

 NA.Issack Gerald-Mpanda Katavi
SHUGHULI Za Uchumi Mkoani Katavi zimesimama kwa siku sita sasa Kutokana na Kukosekana kwa nishati ya Umeme.

Kukosekana kwa Nishati ya Umeme Mkoani hapa Kwa Muda Usiojulikana kumesbabisha Kupanda kwa Gharama za Maisha kutokana na shughuli za Uzalishaji zinazotegemea nishati hiyo kusimama ikiwemo Usafirishaji na viwanda vya ubanguaji na kusindika mazao.
Akizungumza Katika Mahojiano Maalum na  P5 TANZANIA Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania Kituo cha Mpanda Bwana,Chacha Nsiku  amesema hivi sasa Juhudi zinazofanywa na Shirika hilo  ni Kuhakikisha Maeneo ya Huduma Muhimu za Jamii Kama hospitali zinapata umeme.
Aidha bwana  Nsiku ameongeza Kuwa sababu ya Kukosekana kwa Umeme imetokana na Uchakavu wa Mashine zinazotumika kwa sasa ambapo tatizo hilo litadumu kwa Kipindi cha Miezi Mitatu kabla ya Kupatiwa Ufumbuzi.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA