YATIMA MPANDA WAPATA MSAADA,CHANGAMOTO YA FEDHA HALMSHAURI YA WILAYA YASEMA BADO KIKWAZO KUWASAIDIA YATIMA WENGI

Baadhi ya watoto katika picha ambao wamepatiwa msaada
Yatima wakisalimiwa na kupew zawadi ndogondogo

NA.Theressia Lwaji-MPANDA KATAVI
WATOTO yatima 12 kati 32  katika kijiji cha ifukutwa kata ya mpanda ndogo wa halmashauri ya wilaya ya mpanda mkoani katavi  wamepatiwa misaada ya magodoro,vyandarua na blanket.

Akisoma risala kwa kiongozi wa mbio za mwenge afisa ustawi wa jamii halmashauri ya wilaya ya mpanda Bahati Mwailapu amesema halmashauri imetoa msaada watoto hao waliofiwa na wazazi wao ili  kujikinga na ugonjwa wa malaria.
Mwenge wa uhuru Halmshauri ya Wilaya ya Mpanda


Aidha Bw.Mwailapu amesema wanakabiliana na changamoto ya uhaba wa fedha za kuwafikia watoto yatima  wanaoishi katika mazingira magumu wilayani hapa.
Kwa upande wake kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Juma khatibu chum ameitaka jamii kuacha kutelekeza familia ili kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA