JAMII HALMSHAURI YA WILAYA NSIMBO YATAKIWA KUWA KARIBU NA WATOTO KATIKA MALEZI

Baadhi ya viongozi katika Msafara wa mwenge wa Uhuru  wakizuru mandari ya Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo wakati mwenge wa uhuru ulipofika katika halmshauri hiyo

NA.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Jamii katika Halmashauri ya Wilaya  ya  Nsimbo Mkoani Katavi imetakiwa kuwa na ukaribu kimalezi kwa  watoto wao ili kubaini kwa haraka vitendo vya ukatili wakati vinapotokea kwa watoto.

Wito huo umetolewa na Kaimu Afisa Maendeleo ya jamii katika halmashauri ya Nsimbo wakati akizungumza na P5 TANZANIA BLOG kuhusu umuhimu wa Wananchi kutoa  taarifa za vitendo vya kikatili katika idara ya Maendeleo ya jamii katika Halmashauri hiyo.
Bw. Mnubi amesema Wazazi na Walezi kutokuwa na ukaribu  kimalezi kwa watoto wao ni sababu ambayo inachangia jamii kushindwa kugundua kwa haraka vitendo vya ukatili wakati vinapotokea kwa watoto wao.

Wakati huohuo kesi nyingi za kikatiri katika vyombo vya mahakama Mkoani Katavi zimekuwa zikikwama kutolewa hukumu kutokana na kukosekana ushirikiano wa kiushahidi wa kutosha kutoka kwa watendewa kwa jeshi la polisi Mkoani Katavi. 

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA