ZAIDI YA MILIONI TANO ZATUMIKA KUNUNUA VIFAA MAABARA NSIMBO ,WAZAZI WATAKIWA KUTOWAZUIA WATOTO KUSOMA SAYANSI




 
Moja ya vyumba vya maabara Shule ya Sekondari Machimboni
Na.Issack Gerald -Nsimbo Katavi

Wazazi na walezi katika Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi  wametakiwa kutowazuia watoto wao kupata fursa ya elimu.
Wito huo wa kuwataka wazazi na walezi  kutowazuia watoto wao kupata fursa ya elimu hasa katika masomo ya Sayansi umetolewa na Diwani wa kata ya Machimboni ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Elimu,afya  na Maji Halmashauri hiyo Raphael Kalinga  wakati  akikabidhi vifaa vya maabara tatu za Sayansi katika  Shule ya Sekondari Machimboni  iliyopo kata ya Machimboni kwa niaba ya waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda.



Naye Kaimu Mkurugenzi Halmshauri ya Wilaya Nsimbo Michael Nzyungu amesema vifaa hivyo vimegharimu Shilingi milioni tano na laki nne ambapo maabara hizo  zitazinduliwa na Mwenge wa Uhuru utakapowasili keshokutwa  Julai 17 katika Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo ambapo pamoja na mambo mengine wanafunzi wakitakiwa kuvitunza vifaa hivyo.

 Wakati huohuo wazazi kata ya machimboni wamesema kuletwa kwa vifaa vya maabara katika shule hiyo kutaongeza kiwango cha ufaulu wa wanafunzi shuleni hapo.
Vifaa hivyo vinakabidhiwa katika uongozi wa Shule ya sekondari Machimboni ukiwa zikiwa ni wiki tatu tangu maabara hizo kutakiwa ziwe zimekamilika hadi kufikia Juni 30 mwaka huu kama utekelezaji wa agizo la Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete.
Hata hivyo mbali na Gharama ya vifaa hivyo kutajwa,gharama iliyotumika katika ujenzi wa vyumba vitatu vya maabara haijatajwa.


Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA