WALIMU WAPYA MPANDA WATAKIWA KUFANYA KAZI KWA KUZINGATIA WELEDI,KUTOJIHUSISHA NA ANASA KAZINI



Walimu wapya wakiwa katika warsha ya pamoja na maafisa elimu mjini Mpanda

Na.Amosi Venance-Mpanda Katavi
WALIMU wa sekondari wilayani Mpanda mkoani Katavi wametakiwa kuwa na maadili na kufuata weledi katika utendaji kazi ili kuboresha kiwango cha elimu mkoani Katavi.

Afisa elimu sekondari  Bi. Lutungulu Enelia wilaya ya Mpanda ametoa wito huo jana katika semina iliyofanyika katika shule ya sekondari Mwangaza iliyopo mjini Mpanda.

Bi. Lutungulu  amesema kuwa walimu ni kioo cha jamii hivyo wanapaswa wawe na maadili katika utendaji kazi.

Aidha amewaasa kujiepusha na vitendo visivyostahili ikiwa ni pamoja na baadhi ya walimu wasio na maadili kujihusisha na maswala ya rushwa, ngono, na ukosefu wa nidhamu kazini.

Semina hiyo imehudhuriwa na walimu wa shule za sekondari wapya 52 walioripoti katika halmashauri ya mji wa Mpanda.



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA