MTOTO MIAKA 17 AFA MAJI MPANDA




Na.Issack Gerald-Mpanda Katavi
MTOTO aliyefahamika kwa jina la Stanslaus Christopher mwenye umri wa miaka (17) Mkazi wa Mtaa wa Mpadeco Kata ya Makanyagio Wilayani Mpanda Mkoani Katavi, amekufa maji baada ya kutumbukia mtoni katika daraja la Kachoma.

Akizungumza na Mpanda Radio nyumbani kwa Marehemu baba mkubwa wa mtoto huyo,  Gaudens Thadeo amesema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kabla ya kufikwa na mauti katika tukio hilo lililotokea jana.

Naye Mwenyekiti Mtaa wa Mpadeco, Bw. Bernard Nkana, amesema amepata taarifa za msiba huo leo baada ya kurejea kutoka safarini.

Polisi wa kituo cha Wilaya ya Mpanda baada ya kupigiwa simu na mashuhuda waliofika katika tukio hilo walichukua Mwili wa Marehemu na kuupeleka kuuhifadhi katika hospitali ya Wilaya ya Mpanda kusubiri taratibu za mazishi ambapo taratibu za mazishi zimefanyika leo.

Huyo ni mtoto wa pili kufa maji katika familia hiyo ambapo wazazi Mkoani katavi wametakiwa kuwa na uangalizi wa kutosha kwa watoto wao.





Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA