JESHI LA POLISI KATAVI LAWATAKA WANANCHI KUWA MAKINI MITANDAO YA KIJAMII KUHUSU BVR

Na.Mark Ngumba-MPANDA
JESHI La polisi Mkoani Katavi limewataka wananchi Kuwa Makini na Ujumbe unaosambazwa  Katika Mitandao  ya Simu kwa Madai ya Kuhakiki taarifa za watu waliojiandikisha Kupiga kura Kwa Kutumia mashine za Kimtandao BVR.
Tahadhari hiyo imetolewa leo na Kaimu Mpelelezi wa Makosa ya Jinai Mkoa wa Katavi Inspekta Boke Simango wakati akitoa Ufafanuzi wa Makosa ya Kimtandao Katika Kikao kilichowakutanisha walimu wote wa Shule za Msingi Halmashauri ya Manispaa ya Mpanda.

Aidha Inspekta Simango amewataka wananchi watakaopokea Ujumbe wa aina hiyo kutoa taarifa kwa vyombo vya Usalama Wakati huu ambapo Jeshi la Polisi linaendelea na Uchunguzi wake.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA