MGOMO DARADARA MPANDA NAULI KUPUNGUZWA,SUMATRA YASEMA WASIOTAKA NAULI ILIYOPANGWA NA SUMATRA WAPAKI MAGARI


Baadhi ya daradara mjini Mpanda zikiwa zimepaki baada ya madereva  kusitisha safari 

Na.Issack Gerald-Katavi
Madereva wa daradara zinazosafirisha abiria kutoka Mpanda Mjini kuelekea kata ya Kakese leo wamegoma na kumlalamikia Meneja wa mamlaka ya uasafiri wa majini na nchi kavu Sumatra Mkoani Katavi kwa kushusha viwango vya nauli.

Madereva hao wakizungumza na Mpanda Radio wamesema kuwa wamegoma kusafirisha abiria ili kupinga kushushwa kwa viwango vya nauli ambavyo havikidhi gharama za uendeshaji wa magari yao.
Wamesema kuwa nauli imeshushwa kutoka shilingi elfu moja na mia tano hadi elfu moja wakati huo wakisema kuwa gharama ya mafuta basi iendane na kupandishwa kwa viwango vya nauli.
Akizungumza na P5 TANZANIA  Meneja wa Sumatra Mkoa wa Katavi Aman Erasto  ili kujibu shutuma hizo zinazoelekezwa kwake pengine hata katika mamlaka ya usafiri wa majini na nchi kavu kwa ujumla ameeleza msimamo wa Sumatra kuwa wasiotaka kutoza kiwango cha nauli ya shilingi elfu moja basi wapaki magari yao au wahame Mkoa wa Katavi.
Aidha Erasto amesema kuwa watakaotaka kubadilisha barabara za usafiri kutoka Mpanda kuelekea maeneo mengine tofauti na Mpanda kwenda Kakese hawatawapatia Leseni watakazozitaka.

Si mara ya kwanza wamiliki wa vyombo vya usafiri Mkoani Ktavi kugoma kutoa huduma wakitaka masilahi yao kuzingatiwa na mamlaka zinazohusika na utoaji wa huduma wanayoipata ua kuitoa kwa jamii.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA