KIONGOZI MBIO ZA MWENGE MPANDA - ACHENI KUTOA NA KUPOKEA RUSHWA KUPATA VIONGOZI BORA



Na.Issack Gerald-Katavi
JAMII mkoani Katavi imetakiwa kuwafichua wagombea wanaotoa rushwa kupata uongozi katika uchaguzi mkuu utakaofanyika oktoba mwaka huu, ili wapatikane viongozi bora watakaojali maslahi yao.

Wito huo umetolewa jana na Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru  kitaifa Bw. Juma Khatib Chum katika shule ya sekondari ya kasimba wakati akizindua miradi ya maendeleo. 
Muiongoni mwa miradi iliyozinduliwa jana ni pamoja na klabu ya kupinga madawa ya kulevya katika shule ya sekondari Kasimba, wodi ya akina mama kituo cha afya Mwangaza, ofisi ya mtendaji wa kata ya Makanyagio, klabu ya kuzuia maambukizi ya Ukimwi shule ya msingi Katavi.
Mwenge wa uhuru umewasili jana Halmshauri ya Mji wa Mpanda ukitokea Wilayani Nkasi Mkoani Rukwa ambapo leo umeendelea na safari zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na kesho utaelekea Halmshauri ya Wilaya ya Nsimbo na kuhitimisha mbio zake Halmsjhauri ya Wilaya ya Mlele na hatimaye kupokelewa Mkoani Tabora.
Kauli mbiu ya mwenge wa uhuru mwaka huu ni “Tumia haki yako kidemokrasia jiandikishe na upige kura katika uchaguzi wa 2015.”



Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA