WAGOMA KUSHIRIKI SHUGHULI ZA MAENDELEO MPAKA WASOMEWE MAPATO NA MATUMIZI


NA.Issack Gerald-Nsimbo Katavi
Wakazi wa kijiji cha Magamba kilichopo kata ya Magamba Halmashauri ya Wilaya ya Nsimbo Mkoani Katavi wamesema hawatashiriki shughuli mbalimbali za maendeleo zikiwemo  za ufyatuaji tofali za kijiji ikiwa hawatasomewa taarifa ya mapato na matumizi iliyo sahihi.

Wakazi kijiji hao wakizungumza na P5 TANZANIA Kijijini hapo wamesema taarifa ambazo wamekuwa wakisomewa na uongozi wa kijiji chao hazina ukweli ukilinganisha na kile wanachokichangia na kuongeza kuwa mkutano wa mwisho uliofanyika mwezi wa sita ulivurugika kufuatia kutokuwepo maelewano kati ya viongozi na wakazi baada ya taarifa zilizokuwa zikitolewa kutokuwa sahihi.

Kwa upande  wake mwenyekiti wa kijiji cha Magamba Anna Thomas amesema wanatarajia kuitisha mkutano wa dharura kusoma taarifa ya mapato na matumizi kuanzia mwaka 2013 hadi 2014 ili kuondoa utata uliopo.
Hata hivyo pamoja na mambo mengine Afisa Mtendaji Kata ya Magamba George Iresha amesema kuna changamoto ya maandalizi ya mapato na matumizi katika vijiji vilivyo katika kata ya magamba kutokana na kutokuwepo wa maafisa watendaji wa vijiji ambao kimsingi ndio wanaotakiwa kuandaa taarifa hizo.

Suala la kutosoma mapato na matumizi katika serikali za mitaa limekuwa likiibuka katika vijiji na mitaa mingi Mkoani Katavi na kusababisha mgogoro kati ya uongozi na wananchi.


Kwa mjibu wa taratibu za mamlaka za serikali za mitaa hapa nchini ,mapato na matumizi yanatakiwa kusomwa kila baada ya miezi mitatu.

Comments

Popular posts from this blog

HISTORIA FUPI YA ABDULRAHMAN KINANA ALIYEJUZULU UKATIBU MKUU CCM

FAHAMU HISTORIA YA JOKETI ALIYETUMBULIWA NA UVCCM

HISTORIA FUPI YA LAZARO NYALANDU ALIYEIBWAGA CCM NA KUHAMIA CHADEMA